"Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu" (1 Petro 2:9).
Biblia inatujulisha kuwa Mungu ni “nuru” na ni “baba wa mianga”; kwa hiyo, sisi tu wana wa Nuru, tunaishi katika nuru. Hicho ndicho tukisomacho katika sehemu ya mwisho ya mstari wetu wa ufunguzi; tumeletwa katika nuru ya ajabu ya Mungu; hapo ndipo mahali ulipo katika ulimwengu wa roho; unaishi katika nuru Yake-istaajabishayo sasa. Kwa sababu hiyo, hakuna giza kuhusiana na maisha yako.
Kwa uwepesi inaleta katika ufahamu maneno ya Yesu katika Yohana 8:12; Alisema, “…Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.” Tunayo, na inatupasa tuenende katika nuru iyo hiyo ambayo kwayo Mungu anaishi na kutenda. Hii ina maana kwamba tunapaswa kuenenda katika Neno Lake, kwa maana Neno Lake ni nuru (Zaburi 119:105). Kuenenda katika nuru Yake ina maana kwamba ufahamu na mtazamo wako ni matokeo ya Neno; unaona na kuyaishi maisha yako katika taswira [mtazamo] wa Neno pekee!
Neno la Mungu linapaswa kuwa ni nuru pekee ambayo kwayo, na kwa kupitia hiyo unaona. Chini ya nuru hiyo, unaona tu uwezekaniki na ushindi; unauona utukufu wa Mungu; na kwa sababu unauona utukufu, unazungumza na kuenenda ikupasavyo. Pindi unapokubaliana na kile ambacho Neno linachokisema kukuhusu wewe, na kisha ukakiri ipasavyo, unakuwa unaenenda katika nuru ya Mungu. Mungu amekupa Neno Lake ili kuiangaza njia yako, hivyo hakutakuwa na giza au mashaka [wasiwasi/sintofahamu] katika safari yako ya maisha.
Wakolosai 1:12-13 inasema: “Mkimshukuru Baba, aliyewastahilisha kupokea sehemu ya urithi wa watakatifu katika nuru. Naye alituokoa katika nguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake.” Tayari ulishaondolewa kutoka katika giza, na kuhamishwa na kuingizwa katika Ufalme wa Mwana wa pendo la Mungu, ambamo hakuna giza, dhambi, mauti, uovu pia na hakuna mashinikizo ya uharibifu ya ulimwengu huu. Tayari ulishahamishwa na kuingizwa katika neema na uhuru wa kitukufu wa wana wa Mungu. Ona na ishi kutokea katika ulimwengu huo; ni ulimwengu wa ushindi, mamlaka, amani na furaha milele daima.