Katika sehemu nyingi ambapo neno, “Msamaha” limetumika, hakika ilipaswa kutafsiriwa kama “Ondoleo.” Ondoleo maana yake ni uhuru, mfunguo, kutengwa; ina maana kuachalia kosa au makosa kana kwamba hayakuwahi kuwapo [kutendeka]. Kukosa kwako kunachukuliwa kana kwamba haikuwahi kutokea; inatenganishwa na wewe kabisa, na kutenganishwa dhidi ya historia yako. Je, waweza kufikiria hilo?
Mtu anaweza akashangaa, “Hilo linawezekanaje?” Lakini hilo ndilo tulilolisoma katika mstari wetu wa ufunguzi; kuwa Mungu alilitenda hilo sawasawa na wingi wa utajiri wa neema Yake. Hii ina maana kuwa Mungu ana uweza wa kumtenga kabisa mwanadamu dhidi ya dhambi zake kana kwamba hakuwahi kutenda dhambi yoyote, kwa uweza wa damu ya Yesu Kristo! Huo sio msamaha. Msamaha ni kusamehe. Katika kusamehe, unaachiliwa kutopata adhabu, ijapokuwa rekodi inabaki kuwa ulikuwa mkosaji.
Tulipokuwa tunakua katika Ukristo pindi tulipokuwa wachanga kiroho, tulifundishwa baadhi ya mambo ambayo hayakuwa sahihi sana. Moja ya mfano wa mafundisho hayo ilikuwa kwamba mwenye dhambi anapata ondoleo la dhambi, wakati Mkristo anapata msamaha. Hiyo ikimaanisha, pindi unapokuwa umezaliwa mara ya pili, dhambi zako zinakuwa zimeondolewa, lakini baada ya hapo, endapo umefanya kitu cho chote kibaya, unapokea msamaha.
Lakini hebu fikiri kuhusu hilo: endapo ikiwa mwenye dhambi anapata ondoleo la dhambi na dhambi zake zinafutwa [zinaondolewa] kabisa, kwamba hazitakumbukwa tena kamwe, ni kwa nini sasa dhambi za Mkristo ziwe katika rekodi? Mkristo hapaswi kuwa anapokea kitu ambacho ni kidogo kuliko kile ambacho mwenye dhambi amepata. Kile tulichonacho katika Kristo ni ondoleo la dhambi.
Je, ni kitu gani kinachotokea pindi unapokosea? Moja kwa moja unatakaswa kwa damu ya Yesu: “Bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote” (1 Yohana 1:7). Haleluya!
