logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-02-11
WATAKATIFU NA TUSIO NA HATIA

WATAKATIFU NA TUSIO NA HATIA

February 11th, 2019

Kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo (Waefeso 1:4).

 

Waebrania 3:1 inasema, “Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Kristo Yesu.” Je, umetambua ya kuwa tunaitwa “ndugu watakatifu?” ni Mungu pekee anaweza akasema hivyo! Majirani zako, marafiki, ndugu wa familia, n.k, wanaweza wasikuone [wasikuchukulie] kuwa ni mtakatifu; lakini Mungu anasema wewe ni mtakatifu, na uamuzi Wake ndio wenye mashiko. Je, hulifurahii jambo hilo?

 

Wewe si mtakatifu au mwenye haki kwa sababu ya matendo yako, bali ni kwa sababu unaishi katika uwepo wa Mungu, na una asili Yake ya haki. Amekupa haki Yake kama zawadi: “…zaidi sana wao wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki…” (Warumi 5:17). Mbele za Mungu, wewe ni mwenye haki; hakuna rekodi ya dhambi au makosa dhidi ya jina lako. Hii ndio maana amesema hauna hatia.

 

Cha kusikitisha, baadhi hawajaweza kuweka kando laumu zao binafsi. Zimesababishia imani yao na uzima wao kutokuwa na matunda kutokana na hukumu-binafsi; hayo ni makosa. Fikra zako hazipaswi kukuweka katika vifungo vya hukumu na hatia, kwa sababu Yesu, Mwana wa Mungu, alikufa katika sehemu yako. Alilipa gharama kamili kwa ajili ya dhambi zako. Biblia inasema katika Matendo 13:38-39, “…na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa torati ya Musa.”

 

Je, unajua kuhesabiwa haki maana yake ni nini? Inamaanisha umetangazwa kuwa mwenye haki; yaani kukutwa huna hatia; zile hatia zilizokuwa juu yako ziliondolewa kwa sababu hukuwahi kufanya dhambi. Je, hilo linawezekanaje? Ni kwa sababu Yesu alichukua nafasi yako, na sasa u katika nafasi Yake. Je, ni kwa namna gani Mungu anakuona sasa? Anakuona mtakatifu, uliyetakaswa, na uliyetengwa KWA AJILI Yake. Haleluya.

 

Mpaka pale na hadi utakapotambua kuwa Mungu amekufanya wewe kuwa mtakatifu, hutoweza kuishi maisha matakatifu. Unaweza tu kuyaishi maisha ambayo Mungu amekupa. Mbwa anaishi maisha ya ki-mbwa; wanadamu wanaishi maisha ya kibinadamu, kwa sababu wanao uhai wa kibinadamu. Vivyo hivyo, kwa sababu tuna uzima na asili ya Mungu, sisi tu watakatifu na tunaweza kuishi kwa utakatifu. Abarikiwe Mungu!

 

Confession

Baba Mpendwa, ahsante kwa kunifanya nisiye na hatia, mkamilifu, mtakatifu, na nisiye na lawama, na nisiye na hatia mbele Zako katika pendo! Ahsante kwa kifo, kuzikwa na kufufuka kitukufu kwa Kristo Yesu, ambapo kupitia hayo sasa ninasimama nikiwa nimehesabiwa haki mbele Zako, katika Jina la Yesu. Amina.

Further Study

AMPC;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: &

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals