Nanyi pia katika huyo mmekwisha kulisikia neno la kweli, habari njema za wokovu wenu; tena mmekwisha kumwamini yeye, na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu (Waefeso 1:13).
Miaka ya nyuma, kulikuwa na wale waliokuwa wanahubiri na kufundisha kwamba baada ya kuzaliwa mara ya pili, unahitaji “kupigwa mhuri na Roho Mtakatifu.” Kisha wataita watu mbele katika Kanisa, na kuweka mikono juu yao na kutamka, “Tiwa muhuri katika Jina la Yesu.” Katika ufahamu wao, walikuwa wanawatia “muhuri” Wakristo hao. Cha kushangaza waliipata hii kutoka wapi? Kwa sababu Mkristo tayari “alishatiwa muhuri na Roho Mtakatifu” kwa kuzaliwa Upya [mara ya pili].
Sehemu iliyopigiwa mstari katika mstari wetu wa ufunguzi inasema, “…na kutiwa muhuri na Roho yule wa ahadi aliye Mtakatifu” Pindi ulipompokea Roho Mtakatifu, ulitiwa muhuri; kitendo hicho kilifanywa na Roho Mtakatifu; sio kitu cha kitofauti zaidi, au uzoefu mwingine zaidi. Je, kutiwa muhuri kuna maanisha nini, kulingana na Maandiko?
Pindi hati [nakala] inapokuwa imetiwa muhuri, inamaanisha alama au kuna kitu kimeambatanishwa ndani yake kama uthibitisho wa uhalali na umiliki. Kwa mfano, pindi unapoona mhuri wa Rais katika nakala, hiyo ina maana kwamba nakala hiyo imetoka kwa Rais, na ina mamlaka ya Rais. Muhuri pia unamaanisha kuwa muamala fulani umekamilika au kuhitimishwa.
Kuna mambo matatu ambapo kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu kunaashiria: umiliki, ulinzi, na uhalali. Sasa kwa kuwa umezaliwa mara ya pili, na umetiwa muhuri na Roho Mtakatifu, Shetani hawezi kukugusa, kwa sababu kuna chapa [alama] ya Mungu juu yako. Mkono wa Mungu u juu yako. Zaburi 91:7 inasema, “Ijapo watu elfu waanguka ubavuni pako. Naam, kumi elfu mkono wako wa kuume! Hata hivyo hautakukaribia wewe.” Na mstari wa kumi unasema, “Mabaya hayatakupata wewe, Wala tauni haitaikaribia hema yako.” Kwa nini? Ni kwa sababu kuna muhuri wa Mungu juu yako! Chapa hiyo, alama hiyo, inakutenga dhidi ya hatari.
Kama mwana wa Mungu, unalindwa na kuhifadhiwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu. Utukufu Wake umekufunika. Pindi unapolielewa hili, ibilisi hatokuwa na nafasi yoyote katika maisha yako. Hofu haitokuwa na nafasi ndani yako. Endapo utashambuliwa kwa ugonjwa, maradhi au udhaifu, utauamuru utoke kutoka katika mwili wako. Utaishi kila siku kwa ujasiri kuwa hakuna mkakati wowote wa adui unaweza ukatenda kazi dhidi yako, kwa sababu muhuri [chapa] ya Mungu i juu yako. Atukuzwe Mungu!
