logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-02-13
KUKAMILISHWA KATIKA HAKI

KUKAMILISHWA KATIKA HAKI

February 13th, 2019

Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke… (Waefeso 4:11-12).

 

Haki yetu ni haki ya Mungu, kwa hiyo ni kamilifu. Hatukuhitaji kustahili kwa uwezo wetu binafsi; Yesu Kristo ametustahilisha mbele za Baba kuwa washirika wa asili ya Kiungu; ili kuwa washirika wa haki Yake. 2 Wakorintho 5:21 inasema, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.” Hili ni la kuvutia kiasi gani!

 

Baadhi ya Wakristo hawajalielewa hivyo, kwa hiyo, wanajiona binafsi kuwa sio wenye haki na hawajakamilika. Lakini endapo umezaliwa mara ya pili, wewe ni mtakatifu, na hiyo ni asili yako, kwa sababu Yeye aliyekuzaa ni mkamilifu. Waebrania 10:14 inasema, “Maana kwa toleo moja amewakamilisha hata milele hao wanaotakaswa.” Wakolosai 2:10 inasema, “Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka.” Neno “mmetimilika” linamaanisha kukamilishwa; umekamilishwa ndani Yake; Kristo ni utimilifu wako.

 

Unaweza ukataka kuuliza, “Je, mstari wetu wa ufunguzi haudokezi kuwa watakatifu si wakamilifu? Maana unazungumza juu ya “kuwakamilisha watakatifu?” Hapana, mstari huo haumaanishi kuwafanya watakatifu kuwa bora na wakamilifu zaidi; imetafsiriwa kutoka katika neno la Kiyuyani ‘katartismos’ ambalo linamaanisha kuwaandaa au kuwafunza watakatifu kwa ajili ya kazi ya huduma.

 

Fikiri kuhusu hili: pindi mtoto anapokuwa amezaliwa, mtoto huyo anakuwa amezaliwa akiwa mkamilifu kama wazazi wake walivyokamilika. Kisha mtoto anaanza kukua kwa kula vyakula vyenye virutubisho sahihi. Mtoto anahitaji kufunzwa na, kuandaliwa katika maarifa na kwa taarifa sahihi, ili kuweza kutenda kama watu wazima wanavyotenda. Hicho ndicho ambacho mtume Paulo alikimaanisha kwa kusema “kuwakamilisha watakatifu.”

 

Kwa jinsi unavyokuwa unalipokea Neno la Mungu katika roho yako, unakua unaandaliwa kutenda na kuifanya kazi ya huduma; unafunzwa katika maisha ya haki. Haki ya Mungu i katika roho yako, lakini kupitia Neno, unakuwa mahiri zaidi katika mafundisho, ufahamu, na namna ya kuweka katika utendaji haki yako katika Kristo.

 

Confession

Mimi ni mwenye haki wa Mungu katika Kristo Yesu, na ni katika ushirika Naye, ninamiliki na kutawala katika maisha. Ni baraka kuu namna gani, kuwa udhihirisho wa haki Yake na kuzaa matunda ya haki, kwa utukufu wa Jina Lake! Abarikiwe Mungu!

Further Study

; ;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: &

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals