logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-02-14
TULIOCHAGULIWA KWA AJILI YA BARAKA

TULIOCHAGULIWA KWA AJILI YA BARAKA

February 14th, 2019

Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi (Wagalatia 3:29).

 

Mstari wetu wa ufunguzi unasema na kama ninyi ni wa Kristo, basi mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi. Hili linaipinga ile dhana ya kawaida kuwa sio lazima kila mtu awe na mafanikio. Ijapokuwa, kiakili [kihalisia], kila mtu hawezi kuwa na mafanikio, lakini hilo sio miongoni mwa watu wa Mungu, kwa sababu sisi ni warithi wa Mungu na warithi pamoja na Kristo; tayari tumefanikiwa na tumesitawi.

 

Yamkini umetumbukia katika tatizo, kwa sababu tu wewe ni uzao wa Ibrahimu, baraka itakutoa kutoka tatizo au changamoto hiyo; italeta suluhisho au ufumbuzi kwa ajili yako. Endapo una maswali, haraka italeta majibu ndani yako au kukuongoza katika sehemu ambapo majibu yapo. Elewa jambo kuhusiana na baraka; ni athari na matokeo ya uwepo wa Kiungu ndani yako [uwepo wa Mungu ndani yako]. Biblia inasema kuwa Yusufu alikuwa ni mtu aliyesitawi, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye (Mwanzo 39:2); kwa upande wako, ni nzuri zaidi na zaidi: kwa kuwa Anaishi ndani yako!

 

Wengi wa watoto wa Mungu wanahitaji kuja katika maarifa kamili ya Ukristo; wanahitaji kujua ni nini ambacho Mungu ametenda kwa ajili yao, katika Kristo Yesu. Waefeso 1:3 inasema, “Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo.” Tayari umeshabarikiwa kwa baraka “ZOTE” za rohoni katika ulimwengu wa roho, ndani Yake Kristo. Tayari una kila kitu ambacho unahitaji kwa ajili ya maisha ya utauwa: haki, afya, usitawi, ushindi, mafanikio, furaha, amani na kila baraka unazoweza kuzifikiria zote ni zako katika Kristo.

 

Ishi kila siku kwa ufahamu kuwa umebarikiwa; kwamba umechaguliwa na kuitwa katika maisha ya baraka. Fikiri baraka; tamka baraka; na tembea katika baraka.

 

Confession

Ninatamka kwamba mambo yote—afya ya Kiungu, usitawi, mafanikio, furaha, amani, na ushindi—ni yangu, ndani ya Kristo. Nimebarikiwa na ninaishi katika utele, kwa sababu mimi ni uzao wa Ibrahimu. Abarikiwe Mungu!

Further Study

; ;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: &

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals