Ambaye katika yeye tuna ukombozi, yaani, ondoleo la dhambi (Wakolosai 1:14 tafsiri ya EBR).
J e! Haufurahii kwamba katika Kristo, dhambi zetu zote zimeondolewa; za wakati uliopita, za wakati uliopo na za wakati ujao? Hebu fikiri endapo mtu fulani angesema dhambi zetu za wakati ujao hazijashughulikiwa kwa kupitia damu ya Yesu, ni lini sasa Ataenda kuzishughulikia! Ni lini zitakapoondolewa?
Pia, jaribu kufikiri kuwa Mkristo ametenda kosa katika eneo lake la kazi, na kisha akajisemea moyoni mwake, “Hapo ofisini sio sehemu sahihi kwa mimi kuomba sasa hivi; nitaharakisha kumaliza kazi ili niwahi nyumbani nikaombe, na kujipatanisha na Mungu.” Hebu fikiri endapo bado akiwa kazini, ghafla parapanda ikalia kwa ajili ya unyakuo wa Kanisa; je! Ataenda mbinguni au ataachwa?
Sasa, yumkini unawaza, “Mkristo huyo imekula kwake! Hawezi kwenda mbinguni.” Hiyo itaashiria hakika kwamba hujamjua Bwana. Ni mwenye mapenzi makuu mno juu ya wokovu wako kiasi cha kutoweza kukuacha kwa sababu tu umefanya kosa. Ametoa kwa Wakristo kitu kiitwacho kutakaswa otomatiki [moja kwa moja]! Hiki ndicho ambacho Neno linafundisha.
Wale watakao achwa nyuma ni wale ambao hawatembei katika nuru Yake; wale wasiomjua Yeye na wasiompenda. Kitendo tu cha kutambua [kukubali] ya kuwa umekosea, ambacho kutokana na hilo uliazimia kuzungumza Naye, kinaonesha kuwa nuru Yake i katika moyo wako.
Sasa, soma kile ambacho Neno linasema katika 1 Yohana 1:7: “bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.” Sehemu iliyopigiwa mstari haisemi kuwa utatakaswa baada ya kumuomba Mungu msamaha; hapana! Wala haisemi kuwa damu ya Yesu itaenda kukutakasa dhidi ya dhambi; haiko katika wakati ujao; bali ni kitendo cha otomatiki kilicho katika wakati uliopo na endelevu! Damu Yake INAKUTAKASA kila wakati uhitaji [wa kutakaswa] unapoinuka.
Na cha kushangaza ni? Ondoleo hili la dhambi zako lililo la kiotomatiki ni la kisheria mbele za Mungu. Na sio suala la uchaguzi kutoka kwa Mungu; bali ni haki ya kisheria kwa Mkristo. Haleluya!
Hii ndio sababu ni muhimu sana kwamba tujue, tuelewe, na tutembee daima katika nuru ya Neno la Mungu, na sio katika madhanio ya kibinadamu. Tembea katika nuru ya haki yako, ukimpendeza Bwana kwa maisha yako, na hutokuwa na hofu juu ya dhambi, kwa sababu asili yako katika Kristo si mhanga wa dhambi.
![KUTAKASWA MOJA KWA MOJA [OTOMATIKI]](/_next/image?url=https%3A%2F%2Frhapsodyofrealities.b-cdn.net%2Fapp%2Fdailyarticle%2Foct-day-7-practise-eternal-life.jpg&w=1920&q=75)