logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-02-22
USITAWI WA WAKATI WOTE

USITAWI WA WAKATI WOTE

February 22nd, 2019

Nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa (Mwanzo 12:2-3).

 

Kutoka katika Biblia, tunaona hata katika umri wa uzee, Ibrahimu bado alikuwa tajiri, kwasababu Mungu alimbariki katika mambo yote. Alikuwa tajiri katika mifugo, fedha, na dhahabu (Mwanzo 13:2). Neno lililotafsiriwa, “mifugo” ni “wanyama wa shambani”; alikuwa na makundi ya mifugo, kondoo, mbuzi, n.k.

 

Alafu katika Mwanzo 24:1, bado tunasoma kitu kizuri kuhusiana na Ibrahimu; inasema, “Basi Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, na BWANA alikuwa amembariki Ibrahimu katika vitu vyote.” Maisha ya Ibrahimu yaliendelea kutokea utukufu hadi utukufu; hakukuwa na nyakati za kushuka chini. Huu ni mpango wa Mungu kwa maisha yako; kuelekea juu na mbele tu. Hataki ile hali ambapo, mahali fulani katika njia ya maisha yako, utasemwa kama yule aliyewahi kuwa tajiri; ameazimia usitawi wako ukawe wa milele.

 

U mtu mwenye haki wa Mungu, na Biblia inasema, “...njia ya wenye haki ni kama nuru ing’aayo, ikizidi kung’aa hata mchana mkamilifu” (Mithali 4:18). Hiyo ndiyo habari na maendeleo ya maisha ya yule aliye katika Kristo.

 

Hivyo, si tu kwasabu umestaafu basi ndio uwe fukara; Biblia inasema, “Basi hao walio wa imani hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani” (Wagalatia 3:9). Umebarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa mwenye imani, na katika ongezeko la mali na usitawi wako, hakutakuwako na mwisho! Ahimidiwe Mungu!

 

Confession

Mimi ni mrithi wa Mungu na mrithi pamoja na Kristo; dunia ni ya kwangu. Mimi ni uzao wa Ibrahimu; kwahiyo, nimebarikiwa pamoja na Ibrahimu aliye wa imani; nimebarikiwa kwa umande wa mbinguni, kwa utele wa nchi, na kwa wingi wa nafaka na mvinyo. Usitawi wangu hauishi [hauna ukomo].

Further Study

;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: &

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals