logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-02-23
ENENDA (TEMBEA) KATIKA ROHO

ENENDA (TEMBEA) KATIKA ROHO

February 23rd, 2019

Shauri langu ni hili: Ishi kwa uhuru, hai [hodari] na mwenye kuhamasishwa na Roho wa Mungu. Ndipo hutoshurutishwa kuzitimiza tamaa za mwili (Wagalatia 5:16 tafsiri ya MSG).

 

Baadhi ya watu pasipo kukusudia wanaruhusu kila aina ya ugomvi kuota mizizi katika mioyo yao: uchungu, uovu, hasira, wivu, chuki, na kila aina ya ubaya. Lakini Mtume Paulo, katika Kitabu cha Waefeso 4:31-32, alihimiza kuwa tuweke mbali mambo haya yote na kuenenda katika pendo: “Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.”

 

Lakini swali ni, “Je! Inawezekanaje kuenenda katika pendo wakati wote katika ulimwengu ambao kuna chuki sana?” Mstari wetu wa ufunguzi unatupa majibu: “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili” (Wagalatia 5:16). Pindi unapoenenda katika Roho, unaona na kuenenda kwa utofauti; mtazamo wako unakuwa ni wa kitofauti, na kuenenda katika upendo ni jambo la asili kwako. Kuwa uliyezaliwa mara ya pili, una uweza wa kuwapenda watu ambao kikawaida ni vigumu sana au watu ambao wanaonekana si wa kupendeka.

 

Pindi unapoenenda katika Roho, pendo la Mungu huchochewa kutoka ndani yako sana; unakuwa mwenye fadhili na huruma; unaishi maisha zaidi ya kujitazama mahitaji yako binafsi na kuvuka daraja la kibinafsi la kibinadamu na matakwa yako binafsi. Pindi unapoenenda katika Roho, unaenda juu zaidi ya nyanja ya “Hiki ndicho ninachokitaka” au “Hivi ndivyo namna navyopenda kiwe”; unafikiri kiutofauti, na kuwajali wengine kuwa ni bora kuliko nafsi yako mwenyewe (Wafilipi 2:3).

 

Pindi unapoenenda katika Roho, unaona kwa macho Yake na unawaza mawazo ya Kiungu na ya upendo kwa ajili ya wengine. Hakutokuwa na chembe yo yote ya hasira, ubinafsi, uchungu au chuki ikidhihirishwa ndani yako, au kupitia wewe; mambo hayo yatajikuta hayapati nafsi ndani yako. Maneno ya Yesu katika (Mathayo 5:43-44 tafsiri ya KJV) yanakuwa ndiyo muundo [mfumo] wako wa kimaisha: “Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; Lakini mimi nawaambia wapendeni adui zenu, wabariki wale wanaokulaani, watendeeni mema wale wakuchukiao, na waombeeni watesi wenu na wale wanaowaudhi.”

 

Confession

Baba Mpendwa, ninakushukuru kwa ujazo wa Roho Mtakatifu ambao ninaupata kila siku. Mawazo yangu, maneno pamoja na matendo yangu yamehamasishwa kwa pendo Lako, ikinisababisha kuona na kujihusisha pamoja na wengine kwa upendo wa Kristo, katika Jina Lake Yesu. Amina.

Further Study

;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: &

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals