mjazwe Roho [Mtakatifu] na daima [sikuzote] mkiongozwa na Yeye… (Waefeso 5:18 tafsiri ya AMP).
Mwanamke mmoja mpendwa alikuwa na hasira sana juu ya Mkristo mwenzie (dada), na walipokuwa wanarushiana maneno, alimwambia jirani yake, “Neno moja tu zaidi kutoka kwako, nitaangusha hii Biblia, na kukuzaba uso wako!” Wakati huo, hakuwa amebeba Biblia mkononi mwake, lakini alikuwa amemaanisha kwamba ataweka kando kila tahadhari Biblia inayotoa, na kumpiga.
Hilo lina ashiria nini? Lina ashiria kuwa Neno halikuwa katika moyo wake; lilikuwa bado li katika Biblia. Pindi Neno linapokuwa ndani yako, huwezi kulidondosha; ni maisha yako. Kila Mkristo anataka, na anapaswa kuishi, maisha ambayo hutawaliwa na kuongozwa na Roho; maisha ambayo yamejawa na Mungu. Huo ndio Ukristo; Kristo yu hai na anatenda kazi ndani yako; kiasi kwamba daima unakuwa chini ya udhibiti na kanuni za Roho; na si mambo kama hasira, ghadhabu na uchungu.
Kamwe usitawaliwe na fikra au hisia zako; tawaliwa [ongozwa] na Roho. Haijalishi una hasira kiasi gani; jizuilie; katika 2 Petro 1:6 inaitwa “egkrateia” (Kiyunani). Biblia inasema, “Mwe na hasira, ila msitende dhambi…” (Waefeso 4:26). Kwa maneno mengine, “Tawala hasira yako.” Unaweza ukajaribiwa kukasirika, kujaribiwa kutenda kinyume na maisha ya Mkristo; lakini endapo unaenenda katika Roho, hautotimiza kamwe tamaa za mwili.
Ni kwa namna gani unatembea katika Roho? Ni kwa kuishi [kuenenda] katika Neno la Mungu. U ndani ya Kristo sasa; enenda katika upendo. Kuwa unayeongozwa na Roho, na unayetawaliwa na Roho wakati wote. Soma tena mstari wetu wa ufunguzi na uone ni mara nyingi kiasi gani tunapaswa kujazwa kwa Roho: kila siku! Pindi unapokuwa umejawa na Roho, unakuwa na maisha yaliyotawaliwa (yaliyodhibitiwa) na Roho! Haleluya!
