Mungu, akiishamfufua Mwana Wake Yesu, Alimtuma kwenu ninyi kwanza, ili kuwabarikia kwa kumwepusha kila mmoja wenu na maovu yake (Matendo 3:26).
Bwana Yesu alikuja kama baraka kwa ulimwengu, kuwaokoa wanadamu na kuwaleta katika ushirika pamoja Naye, walakini watu wa ulimwenguni hawakumkubali. Hata Wayahudi, ambao kupitia kwao Alikuja, hawakumpokea [hawakumkubali], kwa sababu Alikuja kama mwanadamu. Hakuwa kile ambacho walikitarajia; hawakuwa wakitarajia mtu ambaye anaonekana ni wa kawaida na mwenye kufanana kama wao. Lakini kwa namna yeyote ile Yesu hakuwa ni mtu wa kawaida; Alikuwa ni Mungu Mwenyewe. Vyovyote vile ilivyokuwa, hakuja ulimwenguni kama Mungu.
Wafilipi 2:6-8 inasema, “ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu…bali alijifanya kuwa hana utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena, alipoonekana ana umbo kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba.” Walitarajia mtawala, lakini kwa kuwa walikuwa vipofu kiroho, hawakutambua ya kuwa Yule aliyetembea katikati yao alikuwa ni mtawala wa mbingu na nchi; Mungu Mwenyezi. Walimtarajia Masihi, na Yeye alikuwa ndiye Masihi.
Yesu ni yote yale ambayo Wayahudi na ulimwengu ulikuwa unatafuta na kutazamia, akiwa amefungamanishwa katika kifurushi cha utu wa Kiungu, walakini hawakumtambua. Biblia inasema, “Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea” (Yohana 1:11). Lakini shukurani na ziwe kwa Mungu! Mstari unaofuta wa 12 unasema, “Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake.”
Endapo hujazaliwa mara ya pili, ina maana kuwa hujampokea Yeye; hujaikubali baraka ya Mungu. Yesu ni baraka zote za mbinguni katika mwili; kuwa Naye maishani ni kuwa na kila kitu. Haijalishi ni kitu gani umekuwa ukitafuta katika maisha; kitu gani ambacho umekuwa na uhitaji nacho; mpokee Yesu na utafiti wako, kiu, na kutafuta kwako amani, kutakoma. Yeye ni kituo-kimoja cha duka kwa ajili ya mahitaji yote ya kila kitu cha Kiungu; kila kitu bora [kizuri]; kila kitu cha kimashuhuri ambacho utakihitaji. Yeye ni uzima wako, amani yako, wokovu wako, usitawi wako, hekima yako, haki yako, na kila kitu! Yeye ni baraka ya Mungu kwako! Haleluya!
