logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-02-27
UWEZO, UPENDELEO, NA MWELEKEZO WA KUSITAWI

UWEZO, UPENDELEO, NA MWELEKEZO WA KUSITAWI

February 27th, 2019

Kuna fasiri nyingi za kupendeza za neno, “baraka” au kitenzi “bariki”; mojawapo ni kukirimiwa (kupandikizwa) uwezo, upendeleo, na kuelekezewa katika kusitawi. Pindi unapokuwa umebarikiwa, uwezo wa kufanikiwa unapandikizwa katika maisha yako; unakuwa umeurithi ndani yako na unatenda kazi wakati wote. Una uwezo wa kufanikiwa, kiasi kwamba chochote kile kinachokuhusu kinafanikiwa.

 

Kupandikiza upendeleo maana yake upendeleo wa kiungu hutenda maishani mwako kiasi kwamba hata wapinzani wako husukumwa kukupendelea. Hata pale unapokuwa hautaki kupokea mapendeleo fulani ambayo ni yako; au hauna taarifa za kutosha kuyatamani, upendeleo huo wa Kiungu unayasababisha yakujie. Ni jinsi gani ilivyo muhimu kwako kutambua, na kutembea katika ufahamu huu!

 

Kipengele cha tatu katika fasiri yetu ni kuelekezewa katika kusitawi. Hili lina nguvu vile vile pia, kwa sababu pindi hili linapokuwa limepandikizwa katika maisha yako, utajikuta kwamba daima u katikati kitovu cha mapenzi kamilifu ya Mungu; unaenenda katika uelekeo sahihi, kwa kusudi sahihi, na kwa wakati sahihi. Hata pale unapokuwa huna hata chembe ya dokezo, nguvu hiyo ya kiungu ya baraka hukusababisha au kukuweka katikati ya mapenzi ya Mungu.

 

Kuna watu ambao daima hutumbukia katika matatizo; kunaonekana kana kwamba kuna kitu kinatenda kazi ndani yao kuwasababisha waanguke katika dimbwi la matatizo; lakini sio wewe! Wewe ni mbarikiwa wa Bwana. Kuna upako wa Kiungu unaotenda kazi ndani yako, ambao unakukinga mbali na matatizo na kukutunza katika njia ya uzima; katika njia ya hatma ya Kiungu.

 

Pindi unapokuwa umebarikiwa, hatua zako daima zinakuwa zimeandaliwa [zimeamriwa] na Bwana. Unakuwa msuluhisha tatizo. Baraka huanza kutiririka mara [pindi] tu uingiapo mahala [fulani]! Siku zote unakuwa katika wakati sahihi wa kupendelewa na kuongozwa katika njia ya usitawi. Elementi hizi za baraka hazitendi kazi kwa wakati fulani tu; bali zinatenda kazi daima katika hali endelevu, bila kufeli. Kuwa na ufahamu kuwa ndani yako kuna uwezo, upendeleo, na mwelekezo wa kusitawi, kwa sababu wewe ni mbarikiwa wa Bwana. Haleluya!

 

Confession

Mimi ni pakiti [fundo] la baraka. Nimepokea pandikizo la uwezo, upendeleo, na mwelekezo wa kusitawi. Hatua zangu zinaongozwa na Bwana; niko sehemu sahihi kwa wakati sahihi, nikikutana na watu sahihi, na kufanya mambo sahihi. Daima ni katikati ya makusudi na mpango mkamilifu wa Mungu. Utukufu kwa Mungu!

Further Study

Kumbukumbu la ; ;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: &

2 Year Bible Reading Plan: - 20 &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals