Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye (Yohana 3:17).
Hebu fikiri kuwa una marafiki au ndugu ambao bado hawajazaliwa mara ya pili au watu wanaofanya kazi pamoja nawe ambao hawajazaliwa mara ya pili; usiwaache waende kuzimu! Unahitaji kuugua [moyoni] na kuulilia wokovu wao. Katika sala zako za maombezi, unahitaji kuomboleza na kuomba kwa bidii kwa ajili ya nafsi zao, kwamba nuru ya kitukufu ya Injili iangaze katika mioyo yao. Unahitaji kuwaombea huku ukijua hatari [maafa] yanayowasubiri, mpaka pale utakapokuwa na uhakika wa wokovu wao. Usilichukulie hili kirahisi [kiwepesi].

Fikiri kuhusu wajomba zako na mashangazi; fikiri kuhusu binamu zako, mke wako au mume wako, watoto wako; usiwaache waangamie bila kuwa na Mungu! Usiwaruhusu waende kuzimu! Je! Unajua inamaanisha nini kuwa katika sehemu yenye giza totoro milele yote, na bila kuwa na tumaini la kutoka kamwe.
Uwepo wako nyumbani kwako, shuleni, mahali pa kazi, majirani zako, mtaa, jiji [mji] au nchi sio kwa ajili ya mchezo. Si tu kwa ajili ya wewe kuwa na furaha na kusherekea kuwa wewe umezaliwa mara ya pili; ni lazima ujihusishe na wokovu kwa ajili ya wengine. Wewe ni mwokozi wa ulimwengu wako. Ulitumwa kuwaokoa wengine.
Wewe upo duniani na u hai ili kuitenda kazi ya Bwana; kuwavuna watu wengi zaidi na zaidi waje kwa Yesu Kristo. Tunatakiwa tuwanyakue kutoka kuzimu; baadhi yao wako karibu mno, na endapo hatutowaokoa, watatelezea kuzimu. Ni lazima tuwazuilie [wasitelezee huko].
Bwana ametupa sisi amana ya huduma ya upatanisho, na kwa uaminifu, tunaitenda huduma yetu, tukiwageuza watu kutoka gizani na kuja nuruni, na kutoka katika nguvu za giza na kuja kwa Mungu.