logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-03-15
SHURUTISHWA KWA KWELI YA INJILI

SHURUTISHWA KWA KWELI YA INJILI

March 15th, 2019

Kitu cha kwanza kabisa ambacho kinapaswa kukushurutisha [kukuhamasisha] juu ya kuhubiri Injili ya Yesu Kristo ni kweli ya Injili. Injili sio makisio au hadithi flani za kufikirika. Mtume Petro alisema, “Hatujafuata hadithi zilizotungwa kwa werevu”; Injili hii ni kweli.

 

Pili, maudhui ya Injili, kile inachokisema, kinahamasisha sana: kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi, na kwamba Alikuwa, na ni Mwana wa Mungu katika kweli—Mungu katika mwili. Na kwamba alisulubiwa Msalabani, na Alikufa kwa ajili yetu. Alizikwa, na Mungu alimfufua kutoka katika wafu, na Yu hai leo, na kwamba kifo Chake pale Msalabani ilikuwa ni dhabihu kwa ajili ya dhambi za ulimwengu mzima.

 

Pindi Yesu alipokufa, tulikufa ndani Yake; pindi Alipozikwa, tulizikwa ndani Yake; pindi Mungu Alipomfufua, tulifufuliwa pamoja Naye, na kwa sababu Yeye anaishi, sisi nasi tunaishi. Haleluya! Hizi ni sehemu za usadikisho wetu yaani kuamini kwetu juu ya Yesu na Injili! 2 Wakorintho 5:21 inasema, “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.”

 

Fikiri kuhusu hilo: yule asiyeijua dhambi Alifanywa kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili kwamba sisi tufanywe wenye haki wa Mungu katika Yeye, ambapo sisi tuliokuwa tumekufa kwa sababu ya dhambi, sasa ndani Yake, tunaishi! Ni ujumbe mkuu [Injili kuu] namna gani! Hakuna kitu cha kufanana na hiki katika ulimwengu mzima; ni habari kuu kuliko zote iliyowahi kusimuliwa; habari kubwa inayoshikilia historia ya wakati wote!

 

Sasa, kufikiri kuwa hii ni Injili ambayo Ibrahimu aliitazamia, Isaka na Yakobo na wazee wa zamani waliitazamia na kuitolea unabii! Kitendo tu cha kufikiri kuwa hii ndiyo Injili ambayo tumeikumbatia [tumeikubali]; ambayo imekuwa halisi [dhahiri] sana katika roho zetu; ni jambo la kustaajabisha mno. Ni wimbo usioisha, chemichemi ya furaha isiyo na ukomo.

 

Pindi unapowaza kumhusu Yesu, na kile ambacho Injili inamaanisha, na yote yale Aliyoyafanya kwa ajili yako, unapaswa kuhamasika [kushurutishwa ndani yako] kuihubiri Injili kuliko wakati wo wote ule. Kataa kuwa kimya; simulia kila mahali

 

Confession

Ninasukumwa kwa kweli ya Injili kuhubiri duniani kote. Shauku ya Bwana imenihamasisha kutangaza uhuru kwao waliofungwa, na kuwageuza wanadamu kutoka gizani na kuingia nuruni, na kutoka katika nguvu za Shetani na kuja kwa Mungu. Bwana Mwenyewe anatenda kazi ndani yangu kwa ufanisi— nguvu Yake na shauku—ili kulitimiza kusudi Lake na kumpendeza Yeye katika mambo yote. Amina.

Further Study

; I

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: & Kumbukumbu la

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals