logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-03-17
ISHI KWA IMANI YAKE

ISHI KWA IMANI YAKE

March 17th, 2019

…Na uzima niishio sasa katika mwili, ninauishi katika imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, akajitoa nafsi yake kwa ajili yangu (Wagalatia 2:20 Biblia toleo la KJV).

 

 

 

Pindi Yesu alipokufa msalabani, Alijua ya kuwa endapo tutapata kusikia juu ya pendo Lake, tutaamini na kuwa mmoja pamoja na Yeye. Alikuwa na imani katika kile Alichokitenda, yaani katika dhabihu Yake kwa ajili yetu. Aliamini kuwa tutafanyika kuwa kila kitu ambacho kifo Chake, kuzikwa Kwake, na kufufuka Kwake kutaleta. Hiyo ndiyo imani ya Mwana wa Mungu ambayo kwayo tunapaswa kuishi.

 

Fikiri juu ya hilo katika namna hii: Hebu fikiri kuwa una mtoto ambaye anakaribia kufanya mtihani wake wa mwisho. Na mtihani huo una gharimu sana kiasi kikubwa cha fedha, lakini u tayari kuhatarisha kila kitu. Hivyo, unamwambia mtoto wako, “Mwanangu, hela yote tuliyonayo kwa sasa ndiyo tutakayolipa ili wewe ufanye mtihani wako wa mwisho, lakini hilo si kitu, kwa sababu tunaamini utakuja kufanikiwa, na kwa matokeo yake, mambo yatabadilika katika familia.”

 

Sasa, mwanao anatambua kuwa tumaini la familia nzima liko juu yake; anatambua kuwa anapaswa kufanikiwa [kufaulu] mtihani huu; hawezi kukubali kuiangusha familia. Hivyo, ataitendea kazi imani yako kwake, ambayo itakuwa ndiyo msukumo wake. Rafiki zake wanaweza wakawa wanafanya starehe, lakini yeye atachukua hatua tofauti, kwa sababu anajua umewekeza kila kitu kwake, na kutaka kukufurahisha [kukuridhisha] kwa imani uliyonayo kwake.

 

Hilo Linafanana na Wagalatia 2:20: maisha tunayoyaishi sasa, tunayaishi kwa imani ya Mwana wa Mungu ambaye alitupenda na kuacha yote kwa ajili yetu; hatuwezi kufeli au kumwangusha. Hii ndiyo sababu ni lazima uishi maisha yako kwa utofauti, weka ufahamu wako Kwake, na katika mambo yaliyo juu, na sio katika vitu vya duniani au vya kimwili! Dhamiria kuwa utaishi katika, na kudhihirisha, baraka kamili za Injili ambazo ni zako katika Kristo. Ishi kwa kutimiza ndoto Yake; matarajio Yake; ishi kwa imani ya Mwana wa Mungu!

 

Confession

Nilisulubiwa pamoja na Kristo, lakini ni hai; walakini si mimi tena, bali Kristo yu hai ndani yangu, na uzima niishio sasa katika mwili, ninauishi kwa imani imani ya Mwana wa Mungu, ambaye alinipenda, na kujitoa nafsi Yake kwa ajili yangu! Maisha yangu daima ni kwa ajili ya utukufu Wake! Haleluya.

Further Study

; ;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: & Kumbukumbu la

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals