logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-03-18
UNAMWAKILISHA YEYE

UNAMWAKILISHA YEYE

March 18th, 2019

Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu ye yote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi (Waebrania 4:9-11).

 

Maisha ambayo Kristo amekupa ni yale ya pumziko kamili [halisi] na amani. Haijalishi ni kwa namna gani jinsi ambavyo mambo yamekuwamabaya au magumu, au changamoto unazopitia; ushindi wako umehakikishwa; wewe na Kristo ni mmoja [si wawili], na kwa sababu uko katika muunganiko pamoja Naye, kamwe hauwezi kuwa mhanga; wewe ni mshindi daima na katika kila eneo; wewe hutikisiki.

 

Mwandishi wa nyimbo wa zamani alisema, “Yeye kamwe hakusema utaona jua tu; Yeye kamwe hakusema kuwa hakutokuwa na mvua, lakini hakika Yeye alituahidi moyo uliojawa na nyimbo [moyo wenye kuimba].” Kwa maneno mengine, haijalishi ni kitu gani kimetokea; wewe ni mshindi. Kuna baadhi ya watu hawana hakika ya kile kitakachotokea katika maisha yao; wanaishi katika hofu na mashaka. Lakini katika Kristo, kuna hakikisho [uthibitisho].

 

Warumi 8:35-37 unasema, “Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga? Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa. Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.” Kataa kufadhaishwa na kitu chochote, kwa sababu u katika pumziko la Mungu, na umekoma dhidi ya mihangaiko ya kimaisha. Biblia inasema, “…Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake…” (Waebrania 4:10).

 

Kamwe usimruhusu mtu ye yote au hali yo yote kukuhadaa na kukuchota kwa kukuweka nje ya maisha ya pumziko kamili ndani ya Kristo ambayo umeitwa kuyaishi; ni maisha ya amani pamoja na ustawi. Na kumbuka, njia ya kujishikilia [kujitegemeza] mwenyewe katika maisha haya ya kitukufu ni kwa kuishi kwa imani katika Neno la Mungu; kwa kuliweka Neno katika utendaji katika mambo yote unayoyatenda. Haleluya!

 

Confession

Baba Mpendwa, ninakushukuru kwa pendo Lako lisilo na mwisho kwa ajili yangu; ulizikamilisha kazi zote tangu kuwekwa kwa misingi ya ulimwengu, na kuniitia katika pumziko Lako. Mimi nipo katika pumziko Lako sasa, nikiishi katika amani ya ustawi. Ninakataa kutaabika au kuchanganyikiwa kwa shinikizo la jambo lo lote, kwa jinsi ambavyo niyafurahia maisha yangu ya ushindi maridhawa ndani ya Kristo, katika Jina la Yesu. Amina.

Further Study

;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: & Kumbukumbu la

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals