Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake (1 Yohana 2:15).
Kristo Yesu tayari Ameshakupa kila kitu unachohitaji ili kuwa mshindi, mfanikiwa, na mwenye ustawi katika maisha. Kwa hiyo, hauna sababu yo yote ya kushawishika au kuondoa shabaha yako katika kuutimiza mwito Wake katika maisha yako.
Vishawishi vinaweza kuja katika njia tofauti-tofauti ili kuzorotesha shauku yako, na kukuzuia kuwa yale yote ambayo Bwana amekukusudia uwe. Vishawishi hivyo vinaweza kuja katika mfumo wa mahitaji; mambo unayotaka au mambo unayotaka kufanya, pasipo kujali yanatenda kazi au la. Vishawishi pia vinaweza kuja kutoka kwa watu kama ndugu, wazazi, marafiki, ambao wanajaribu kuihamisha shabaha yako kwenda katika kitu kingine ambacho ni tofauti na mwito wa Mungu katika maisha yako.
Hata hivyo, kwa njia yo yote au katika kivuli chochote kile cha ushawishi kinachotumika kukujia, kataa kuviruhusu. Tambua kuwa kama Mkristo, haswa pale ambapo unasababisha athari kwa kupitia Injili, utakumbana na udhia [mateso]; kutakuwa na wale watakaokuwa kinyume chako, au hata kukuchukia, lakini hilo kamwe halipaswi kuwa ni kitu cha kukushangaza hata kidogo. Yesu alisema, “Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi pia” (Yohana 15:20). Lakini nikuambie kitu? Haijalishi, ni nani aliye kinyume chako. Wewe ni mshindi milele; wewe ni zaidi ya mshindi.
Vishawishi vinaweza vikatoka kwa ibilisi pia. Anaweza akaleta mawazo kwako kama ya, “Unafikiri unatakiwa kuwa Mkristo? Huu Ukristo umewahi kukufanyia kitu gani?” Kamwe usikae kuendekeza mawazo ya namna hiyo; pindi yanapokuja, yapinge na tamka. “Toka hapa, Shetani, kwa maana huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
Endelea kulichochea pendo lako kwa Bwana, na kataa kuruhusu kitu chochote kuharibu bidii [shauku] yako: chochote kile ambacho kitakuzuia kuweka ubora wako wote katika Injili. Mara tu utakapokuwa umeweza kuondoa vishawishi katika maisha yako, utaona maboresho ya ajabu katika utu wako, matokeo na ushawishi. Dumisha shabaha yako; kuwa bora kabisa kwa kiwango cha juu kwa ajili ya Bwana na Ufalme Wake wa milele.
