Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu (Warumi 6:23).
Baadhi ya watu hufikiri tu hasira ya Mungu; wanaamini kuwa Anafukuta kwa hasira juu ulimwengu kutokea mbinguni, Akiitazamia siku ile ambayo hatimaye Atamhukumu mwanadamu na ulimwengu huu wa dhambi; hapana! Mungu hajali tena kuhusiana na dhambi kama vile ambavyo wengi wanafikiri. Alijali sana kuhusiana na dhambi, na kwa kujali Kwake alituma Yesu.
Leo, msisitizo hauko tena katika mshahara wa dhambi, ambao ni mauti, bali katika karama ya Mungu, ambayo ni uzima wa milele kupitia Kristo Yesu (Warumi 6:23). Mungu anataka ulimwengu mzima upokee wokovu ambao tayari Ameshafanya upatikanike katika Kristo Yesu. Biblia inasema kuwa Yeye hapendi mtu ye yote apotee, bali wote waifikilie toba (2 Petro 3:9).
Pindi Yesu alipokufa pale msalabani, tatizo la dhambi lilitatuliwa milele. Hivyo, dhambi si tatizo tena. Mauti, kuzikwa, na kufufuka kwa Yesu Kristo kulileta ukomo wa dhambi na kutuingiza katika maisha ya haki: “Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye” (2 Wakorintho 5:21).
Mungu hana hasira juu yako; Alitatua changamoto ya tatizo-la-dhambi katika, na kwa kupitia Kristo Yesu. Sasa unaweza kumfurahia kwa kile Alichokisema, “Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi…” (Warumi 6:14). Kile unachopaswa kufanya ni kuiamini haki Yake; amini kile Yesu alichokuja kukifanya! Wewe ni matunda— yaani matokeo ya kazi ya ukombozi wa Kristo. Kubali na enenda katika haki Yake, na ishi daima katika pendo Lake, utukufu Wake, na neema Yake.
2 Wakorintho 5:19 unasema, “Yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho.” Fikiri kuhusu hilo: Mungu wala hata hana hasira na mtu mwenye dhambi, achalia mbali wewe ambaye ni mzao Wake! Kwa hiyo, furahi na shangilia; Baba yako wa mbinguni anakupenda, na kamwe hakushutumu kuwa unawajibika kwa dhambi zako. Biblia inasema, “Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake” (Warumi 5:10). Ni wa rehema na fadhili kuu kiasi gani!
