logoRhapsody Today
Read RhapsodyTopicsQuizSearch
Overcoming FearFreedom from WorryOvercoming DoubtFinding HopeFinancial WisdomWalking in Peace

© 2026 Rhapsody Today

QuizPrayer of SalvationFAQAbout

Daily Devotional

Rhapsody of Realities

2019-04-05
PEPEA MOTO WA FURAHA YAKO

PEPEA MOTO WA FURAHA YAKO

April 5th, 2019

Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini (Wafilipi 4:4).

 

Furaha ni tunda mojawapo la roho ya mwanadamu iliyoumbwa upya, kitu ambacho ni cha asili ndani yako. Hivyo, haijalishi ni taarifa gani au tukio gani linalojaribu kukufanya kuwa mtu usiye na furaha; daima unaweza kuwa na furaha katika Roho Mtakatifu, kwa maana hivyo ndivyo ulivyo Ufalme wa Mungu. Warumi 14:17 unasema, “Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.” Waefeso 5:18-19 unafunua ni kwa jinsi gani unavyoweza kuwa uliyejaa furaha katika Roho Mtakatifu daima; “Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu.”

 

Hii ni mojawapo ya siri za mafanikio ya Mtume Paulo; aliandika kile ambacho tumesoma katika mstari wetu wa ufunguzi, wakati akiwa gerezani. Alikuwa amejawa na furaha, na kuendelea kuhubiri Injili gerezani. Katika barua yake kwa Kanisa la Uefeso, alisema, “Mniombee ’…ili nifungue kinywa changu kwa ujasiri, kuihubiri ile siri ya Injili, ambayo kwayo mimi ni mjumbe [balozi] katika vifungo: ili ndani yangu ninene kwa ujasiri, kama inipasavyo kunena’” (Waefeso 6:19-20 Biblia toleo la KJV). Tazama sehemu iliyopigiwa mstari; hakuruhusu kile anachopitia kitawale hisia zake au kiingilie furaha ya Bwana katika roho yake. Katika maisha yako, ona changamoto kama fursa kwa ajili ya kuinuliwa kwako, na kwa ajili ya kudhihirisha utukufu wa Mungu; kwa njia hiyo, daima utakuwa umejawa na furaha wakati wote. Yakobo 1:2 unasema, “Ndugu zangu, hesabuni ya kuwa ni furaha tupu, mkiangukia katika majaribu mbalimbali.” Warumi 8:28 unasema, “Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.”

 

Neno linapaswa kuunda msingi wa furaha yako wakati wote. Pindi unapozitafsiri na kukabiliana na changamoto mbalimbali kulingana na msingi wa Neno la Mungu, utagundua kuwa hakuna kitu katika maisha ambacho kinaweza kikakusababishia kuwa na siku mbaya au kikufanye kuwa mhanga, kwa sababu furaha inakuja kupitia Neno na Roho wa Mungu.

 

Confession

Bwana Yesu, kupitia kifo Chake kwa niaba yangu na kukufuka Kwake kitukufu, kumenileta mimi katika maisha ya furaha isiyo na ukomo, ushindi, utawala na haki; na kwa ajili ya hili, ninafurahi daima milele, tena kwa furaha isiyoneneka, na iliyojawa na utukufu. Furaha yangu ni ya Roho Mtakatifu, na kwa kupitia Neno; hivyo, haina mipaka. Haleluya!

Further Study

; ;

Bible Reading Plan

1 Year Bible Reading Plan: &

2 Year Bible Reading Plan: &

Not sure about your relationship with God?

Previous Devotionals